Kuna hadithi Fulani ya zamani ila kwa leo naona inanipa
maana kuliko wakati naisikia.
Kulikua na mtu mmoja,
mtumwa aliyekua anafanya kazi kwa mfalme. Alikua na bidii sana na mfalme
alimpenda sana. Hilo lilimfanya mtumwa huyo kuishi rah asana na kujivunia kuwa mtumwa wa mfalme.
Siku
moja ndugu zake walikuja kwa mfalme na kutaka kumkomboa kwa kulipa gharama kwa
mfalme ili waondoke naye na awe huru.
Kabla hata hawajafika kwa mfalme Yule mtumwa alikataa kata
kata. Aliwaza yanini nikaanze tena maisha ya kutafuta ardhi, nitafute chakula changu
mwenyewe, heri kuendelea kula na kulala hapa hapa kwa mfalme.
Siku moja mfalme akafa. Ki utaratibu wa kule ilikua mfalme
akifa hawezi kuzikwa peke yake. Anazikwa pamoja na mtumwa aliyempenda. UNAJUA
KILICHO FUATA.
MAANA YAKE.
Usiishie kufurahia kufanya kazi kwa mtu. Heri kuanza
kujizoeza kutafuta chakwako. Hata kama ni vigumu lakini malipo yake ni makubwa.
Unafurahia kuwa mfanyakazi bora na unayependwa na wenye
ofisi.
Lakini ujue siku ofisi ikifa, na wewe unakufa.
Tumeona wengi sana waliokuwa wanafanya kazi kwenye makampuni
makubwa na madogo. Kampuni ikifa au ikibadilika wanakuwa hawana tena kazi.
Hivi leo mimi ndugu yako ndo nakuja na ujumbe wa kutaka
kukukomboa kabla mfalme hajafa.
Anza kujilipia uhuru wako ndugu yangu. Kuna siku mfalme
atakufa.
© Grant Sumaye
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.