0

Kuna hadithi Fulani ya zamani ila kwa leo naona inanipa maana kuliko wakati naisikia.

Kulikua na  mtu mmoja, mtumwa aliyekua anafanya kazi kwa mfalme. Alikua na bidii sana na mfalme alimpenda sana. Hilo lilimfanya mtumwa huyo kuishi  rah asana na kujivunia kuwa mtumwa wa mfalme. 

Siku moja ndugu zake walikuja kwa mfalme na kutaka kumkomboa kwa kulipa gharama kwa mfalme ili waondoke naye na awe huru.

Kabla hata hawajafika kwa mfalme Yule mtumwa alikataa kata kata. Aliwaza yanini nikaanze tena maisha ya kutafuta ardhi, nitafute chakula changu mwenyewe, heri kuendelea kula na kulala hapa hapa kwa mfalme.

Siku moja mfalme akafa. Ki utaratibu wa kule ilikua mfalme akifa hawezi kuzikwa peke yake. Anazikwa pamoja na mtumwa aliyempenda. UNAJUA KILICHO FUATA.

MAANA YAKE.

Usiishie kufurahia kufanya kazi kwa mtu. Heri kuanza kujizoeza kutafuta chakwako. Hata kama ni vigumu lakini malipo yake ni makubwa.

Unafurahia kuwa mfanyakazi bora na unayependwa na wenye ofisi.
 Lakini ujue siku ofisi ikifa, na wewe unakufa.

Tumeona wengi sana waliokuwa wanafanya kazi kwenye makampuni makubwa na madogo. Kampuni ikifa au ikibadilika wanakuwa hawana tena kazi. 

Hivi leo mimi ndugu yako ndo nakuja na ujumbe wa kutaka kukukomboa kabla mfalme hajafa.

Anza kujilipia uhuru wako ndugu yangu. Kuna siku mfalme atakufa.

© Grant Sumaye


Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post a Comment

 
Top