BIASHARA YA MTANDAO
Watu wengi sana leo
wanaishi maisha yasiyo kuwa na ndoto kabisa. Hii ni kutokana na maisha yalivyo
na mfumo wa uchumi umewafanya wasione kabisa uwezekano wa kuzifikia ndoto zao.
Sio kwamba hawajawahi
kuwa na ndoto, hasha. Ila ndoto zao zimeuawa na mfumo au niseme ugumu wa
maisha. Wengine hata hawazikumbuki tena ndoto walizowahi kuwa nazo.
Hebu jiulize, kama
fedha isingekuwa kikwazo je:-
Ø Hiyo nyumba unayoishi ndiyo
ambayo ungeishi?
Ø Ungevaa kama unavyo vaa
leo?
Ø Ungefanya nini kwa wazazi au ndugu
zako wasio na uwezo?
Ø Ungejitoa kiasi gani kwa ajili ya
Mungu?
Ø Ungetaka kufika wapi na wapi duniani?
Utagundua wengi tunaisha
maisha ambayo siyo ndoto zetu ila tumeamua kuyakubali kwa sababu hatuoni namna
nyingine.
Wengi tuliweka tuliamini
kuwa pengine kukipata kazi mambo yatakuwa sawa, lakini baada ya kupata kazi
mwaka wa kumi sasa mambo bado ni magumu.
Leo nataka nikuoneshe
fursa ambayo wengi hawajaiona. Na hii ni fursa ya kujiajiri bila kuathiri ajira
yako ya sasa.
Fursa hii ni kufanya
biashara kwa muda mfupi sana kwa siku na katika masaa ya ziada.
Fursa hii kama ikitumiwa
vizuri na kwa juhudi inaweza kufufua upya ndo zako.
Hapa nazungumzia kufanya biashara ya mtandao yaani
NETWORK MARKETING.
Najua wengi wamewahi
kusikia kuhusu biashara ya mtandao ila naomba uchukue nafasi hii tena kuifahamu
zaidi.
Hata kama hutaki kufanya
biashara hii nakushauri usome tu na kuilewa, pengine siku moja unaweza kuamua
kufanya au hata kumsaidia mtu mwingine
BIASHARA NA MTANDAO NI
NINI?
Biashara ya mtandao au
network marketing ni mfumo mpya wa usambazaji na ugavi wa bidhaa
unaoshamiri kwa kasi kwenye karne hii ya 21.
Mfumo huu ulianza mwaka
1950 huko Marekani. Kuna makampuni mengi sana duniani kwa sasa
ambayo yamesajiliwa kufanya biashara kwa njia hii ya mtandao.
Mfumo huu unamruhusu
mteja mwenyewe kuwa ndio msambazaji na muuzaji wa bidhaa.
Kwa mfumo huu, unakuwa
umepunguza wauzaji waliopo kati ya kiwanda na mtumiaji, kama vile, wakala mkuu, wauzaji wa jumla,
wenye maduka kisha mtumiaji.
kwa kifupi kwenye
biashara ya mtandao, mteja ndiye anayekuwa msambazaji na mtangazaji wa bidhaa
na kampuni inamlipa kamisheni kwa kadri ya manunuzi wateja
aliyowatambulisha bidhaa.
kama ambavyo unaweza
kumwelekeza rafiki yako kwenye saluni nzuri, au mgahawa mzuri au hata duka
zuri, unaweza pia kumwelekeza rafiki yako au ndugu yako kwenye bidhaa nzuri.
tofauti na saluni au
mgahawa au duka ambao hawatakupa chochote hata kama mteja ulimwelekeza atanunua
vitu vya milioni moja, kwenye biashara ya mtandao kila kitu atakachonunua mteja
uliyemweleza wewe, utapata kamisheni ya asilimia fulani.
FAIDA ZA BIASHARA YA
MTANDAO
Ø Utaifanya kwa muda wa ziada bila
kuathiri kazi au biashaza yako nyingine.
Ø Unaweza kuanza na mtaji mdogo sana
Ø Huta kuwa umeajiriwa
Ø Huta hitaji wafanya kazi.
Ø Hulazimiki kukaa na bidhaa nyumbani
kwako au kwenye duka.
Ø Utajifunza elimu ya ujasiriamali
kuliko ukiwa mahali pengine popote.
Ø Utapata bonas/gawio kila mwezi kulinga
na manunuzi yako pamoja na manunuzi ya watu ulio waelekeza
Ø Inakupa uhuru wa kweli wa muda.
Unaweza kuwa huru bila kazi lakini ukawa unaingiza fedha.
Ø Utaingiza fedha kulingana na juhudi
zako na sio kulingana na muda.
Ø Haina kulipa kodi kwani kodi hulipwa
na kampuni husika.
© Grant
+255 763 449 749
Facebook: Grant Sumaye
Instagram: grant_s.s
☆Change first. Change
fast.☆
Post a Comment